
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Omar, amezitaka Taasisi na Mashirika mbalimbali ya elimu kuimarisha usimamizi na uongozi wa elimu ili kuwezesha kikamilifu utekelezaji wa sera ya elimu na Mafunzo ya 2014 Toleo la 2023.
Dkt. Omari ametoa rai hiyo Oktoba 3, 2025 mkoani Morogoro akizundua Jukwaa la Kitaaluma la Wadau wa Uongozi na Usimamizi wa Elimu Nchini, lililoandaliwa na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), ambapo amesema jukwaa hilo litaisaidia Serikali na wadau kuwa na sauti moja, kurahisisha uratibu na kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali katika sekta ya elimu.
“Kupitia jukwaa hili, tutajua taasisi ipi inafanya nini na wapi, jambo litakalosaidia kuunganisha jitihada za wadau na kuleta matokeo chanya katika elimu,” amesema Dkt. Omar.
Makamu Mkuu wa Chuo ADEM, Dkt. Emmanuel Mollel, amesema Jukwaa hiilo ni fursa ya kujenga mshikamano kati ya taasisi zinazoshughulika na uongozi wa elimu na elimu kqa ujumla, kushirikiana katika tafiti na kubadilishana utaalamu.
“Tunashukuru kupata nafasi ya kukukutana na wadau wanaofanya kazi zinazofanana katika eneo hili la elimu nchinj. Hii itarahisisha kushirikiana katika matumizi ya rasilimali na kuwa na mwelekeo mmoja ili kufukia malengo mapana ya maendeleo ya Elimu Kitaifa,” ameeleza Dkt. Mollel.
Naye, Kiongozi wa Mradi wa Shule Bora, Virginie Briand, amesema kuwa mradi huo unachangia kuwezesha mafunzo ya kwa viongozi wa shule ili kuwajengea uwezo wa kupanga na kuongoza kimkakati na kukuza utamaduni bora wa kujifunza.