Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Agosti 25, 2025 amekagua maonesho ya wadau wa Elimu ya Watu Wazima katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) yaliyofanyika JNICC jijini Dar es Salaam.



Maonesho hayo yamewaleta pamoja wadau mbalimbali kutoka sekta ya elimu, mashirika ya maendeleo, taasisi za kijamii na washiriki binafsi, wakionyesha mchango wao katika kuendeleza elimu jumuishi na ujuzi kwa watu wazima nchini.