
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amesema viongozi bora ni chachu ya utekelezaji wa mageuzi ya elimu nchini ambayo yatasaidia kupata wahitimu mahiri wenye uwezo wa kushiriki katika maendeleo ya taifa.

Akizungumza Novemba 18, 2025 jijini Dodoma, Prof. Nombo amewapongeza viongozi wapya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Wanu Hafidh Ameir, akisema kuwa uteuzi wao na kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni ishara ya kuaminiwa kwa uongozi wao mahiri.

Aidha, Prof. Nombo amesisitiza kuwa Wizara inajivunia viongozi hao na ipo tayari kushirikiana kikamilifu katika utekelezaji wa mageuzi ya elimu nchini.

Prof. Nombo amewaongoza Watumishi katika hafla ya mapokezi ya viongozi hao, ambapo wamepokelewa rasmi na kuahidi kushirikiana katika safari ya mageuzi ya elimu.

