
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI (Elimu) Ndg. Atupele Mwambene amesema kupitia Mkutano wa Mwaka wa Tathimini ya Pamoja Sekta ya Elimi, washiriki wamefanya tathimini ya kina kuhusu utekelezaji wa Sera ya Elimu, na kwamba imebanika kuna mafanikio makubwa yaliyofikiwa.

Mwambene amesema hayo Oktoba 24, 2025 jijini Dodoma ambapo ameongeza kuwa Mkutano huo umekuwa nyenzo kubwa ya kuwakutanisha wadau mbalimbali, ambapo michango yao ya kitaalam yatawezesha kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa Sera ya Elimu.

"Sisi kama sekta ya elimu bado tuna fursa za kufanya vizuri zaidi, kwa kuboresha na kuimarisha utendaji katika upande wa elimu ya awali, Msingi na Sekondari ili tuongeze fursa za upatikanaji wa elimu kwa vitendo" amesema Mwambene.

Jumla ya Washiriki 367 wakiwemo Wadau wa Maendeleo, Sekta Binafsi, FBOs, Taasisi za Elimu ya Juu, Walimu wa shule za Msingi na Sekondari wameshiriki kikamilifu katika Mkutano huo.


