Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ikipata maelezo ya vifaa na mitambo ya kisasa ya kufundishia na kujifunzia katika karakana ya Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Wilaya ya Chemba januari 24, 2026.



Mitambo na vifaa hivyo vimenunuliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kusambazwa katika vyuo 54 vya VETA nchini.



Vifaa na mitambo hiyo vimewezesha kuimarisha ubora wa mafunzo ya ufundi stadi na mafunzo ya ujuzi kwa vitendo kwa kutumia teknolojia za kisasa, na kuwaandaa wahitimu kuwa na uwezo wa kushindana katika soko la ajira la ndani na kimataifa.