
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zuber Ali Mbwana, ameipongeza Taasisi ya Lalji Foundation kwa jitihada za kutoa misaada kwa watoto yatima na wasiojiweza, akisisitiza kuwa ni matendo yenye thawabu kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.

Kiongozi huyo ametoa pongezi hizo Januari 10, 2026 jijini Dar es Salaam katika hafla ya ugawaji wa vifaa mbalimbali kwa wanafunzi kutoka vituo vya kulea watoto yatima, chini ya ufadhili taasisi hiyo.

Kwa upande wake Mlezi wa Taasisi hiyo Ndg. Mohsin Lalji amesema kuwa Taasisi imewazawadia watoto 400 wa shule za Msingi vifaa vya shule ikiwemo sare.

Ameongeza kuwa katika kuchangia juhudi za Serikali katika sekta ya elimu, Taasisi imechangia madawati 300 kwenye shule zenye uhitaji.


