Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Mohamed Omar, tarehe 22 Julai 2025, amefanya ziara katika Ofisi za Baraza la Mitihani la Tanzania zilizopo jijini Dar es Salaam.



Katika ziara hiyo, Dkt. Omar alipata fursa ya kukutana na uongozi wa Baraza na kujionea namna taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake, hususan katika eneo la matumizi ya TEHAMA katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali.



Dkt. Omar amepongeza juhudi zinazofanywa na Baraza katika kuimarisha mifumo ya TEHAMA, na kuwahimiza kuendelea kujikita zaidi katika matumizi ya teknolojia ya kisasa ili kuboresha ufanisi wa utendaji kazi.



Aidha, amelitaka Baraza kuzingatia zaidi uundaji wa mitihani inayolenga kupima umahiri wa wanafunzi ili iendane na mabadiliko ya mitaala na mahitaji halisi ya soko la ajira