Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa Shule, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ephrahim Simbeye, atoa wito kwa wadau wa elimu na wazazi kuimarisha usimamizi na uwajibikaji ili kuwawezesha wanafunzi kukamilisha mzunguko wa masomo momba.



Katika hotuba yake ya kufunga Juma le elimu mkoani songwe, Dkt Ephrahim Simbeye, akimuwakilisha Katibu Mkuu wizara ya elimu Sayansi na Teknolojia amewataka wadau wa elimu kuimarisha uwajibikaji hasa wazazi kwa kushiriki kikamilifu katika elimu ya watoto kwa kuhakikisha wanawaandikisha na kuwasimamia kukamilisha mzunguko wao wa masomo. Pia ameitaka sekta binafsi kuwekeza katika elimu na AZAKI kuendelea kuhamasisha mabadiliko ya kijamii akisema kuwa jitihada hizi zitakua ni zao la taifa lililo na raslimali bora na lenye maendeleo.



Aidha, Dkt. Simbeye amesema kuwa wakati wa ziara zilizofanyika na wadau shuleni, tumeona mambo mbalimbali mazuri yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akisisitiza namna midahalo ya kijamii, na majadiliano ya wadau, yalivyochangia katika kuongeza uelewa wa kina kuhusu hali halisi ya elimu katika Wilaya ya Momba na Mkoa wa Songwe kwa ujumla.



Pia uamuzi wa Dkt Simbeye kutatua changamoto ya dereva katika shule ya sekondari ya Amali Msangano umewafurahisha wadau, waalimu na hasa wanafunzi wa shule hiyo kwani ameagiza dereva apelekwe shuleni hapo mara haraka iwezekanavyo ili kuwezesha wanafunzi kujifunza kwa urahisi Zaidi matumizi ya vifaa hivyo vya amali.