
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, tarehe 27 Januari 2026, amekutana na Ms Anna Wilson, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza (FCDO).

Lengo la kikao hicho kilikuwa ni kujitambulisha pamoja na kumpitisha mgeni huyo katika majukumu na kazi mbalimbali zinazotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika kuendeleza sekta ya elimu nchini.


