Hii si ndege ya kubeba abiria bali ni kati ya vifaa vinavyotumika kutoa mafunzo mbalimbali kwa wataalamu wa sekta ya anga ambapo takriban shilingi bilioni 49 zimetolewa kwa ajili ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kununua vifaa hivyo na ujenzi wa kituo cha umahiri.Hiki ni kishindo cha Mradi wa Afrika Mashariki wa Kujenga Ujuzi kwa Mlingano na Ulinganifu wa Kikanda (EASTRIP) ulio chini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na kufadhiliwa na Benki ya Dunia.Ukifika NIT utakunana na kazi kubwa inaendelea ya ujenzi na pia vifaa vya kisasa vya mafunzo katika nyanja ya usafirishaji wa anga.Vifaa hivi vyenye muundo wa ndege halisi kitaalamu vinaitwa _Mock ups, ni za ndege aina ya Boeng 737 Dash 800 hapa nchini utavikuta katika chuo hicho cha NIT.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan anaendelea kuimarisha Shirika letu la Ndege ATC na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaendelea kuhakikisha watalaamu wenye ujuzi wanaendelea kuandaliwa hapa nchini katika viwango vya kimataifa.Hii ni sehemu tu ya utekelezaji wa Mradi huu wa EASTRIP kupata taarifa zaidi juu ya nini kimefanywa na Mradi huuEndelea kutufuatilia katika mitandao yetu ya Kijamii