
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali imedhamiria kufanya mageuzi ya elimu, sayansi, utafiti na ubunifu ili kujenga uchumi imara na endelevu.

Mhe. Samia amesema hayo Januari 8, 2026 baada ya kuzindua Jengo la Taaluma na Utawala la Taasisi ya Sayansi za Bahari Zanzibar Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM - MSI). Amesisitiza kuwa Taasisi hiyo, ni mdau muhimu kwa Serikali katika kujenga uchumi shindani na shirikishi.

Mhe. Rais ameongeza kuwa Taasisi hiyo ya kimkakati itachangia uvuvi endelevu, utalii wa bahari na uchumi wa Bluu.

Ameipongeza Wizara ya Elimu Syansi na Teknolojia kwa kusimamai mradi wa HEET kwa ufanisikubwa na kuleta matokeo chanya huku akiwataka vijana kutumia fursa uwepo wa. Huo hi ho kusoma ili kupata elimu na ujuzi.

Katika hatua ingine amepongeza viongozi na Watumishi wa UDSM kwa kukamilisha mradi huo kwa wakati na ufanisi na ameishukuru Benki ya Dunia kwa kushikiana na Serikali katika kutekeleza mradi wa Mradi wa HEET.

Amewataka Wahadhiri na watafiti kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi kuleta maendeleo, na amewahimiza wanafunzi kujifunza kwa bidii, kuwa mabalozi na walinzi wa rasilimali za bahari.

