Mkurugenzi wa Elimu Maalumu kutoka wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt Magreth Matonya amesema Serikali imetoa Mwongozo wa Shule Nyumbani ili kuhakikisha watoto wenye ulemavu ambao hawawezi kwenda shule walimu wanawafuata majumbani na kuwafundisha kama wanavyofundushwa shuleni na baadaye kutahiniwa kama wengine.



Dkt Matonya amesema kuwa Mwongozo huo uliandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia baada ya kufanya ufuatiliaji katika maeneo mbalimbali na kubaini kuna wanafunzi ambao wanabaki majumbani kwa kushindwa kwenda shuleni kutokana na changamoto za viwango vya juu vya ulemavu au afya.



Ametoa mfano mwanafunzi aliyefanya mtihani wa darasa la nne akiwa hosipitalini na matokeo yalipotoka alipata masomo yote alama za A. ameongeza kuwa mpaka sasa kuna wanafunzi 26 wanaosoma katika mfumo wa Shule ya nyumbani katika Mikoa ya Dar es Salaam. Mwanza Tanga, Mbeya na Arusha.