Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imethibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), kuwa na mifumo ya usimamizi kwa hadhi ya Kimataifa katika kundi la Taasisi za Elimu, Education Organizations Management System (EOMS) – ISO 21001:2018.



Hatua hiyo inaonesha dhamira ya taasisi katika kuimarisha ubora na ufanisi wa huduma za elimu nchini.



Akizungumza katika hafla hiyo Naibu Katibu Mkuu -Elimu, Dkt. Hussein Mohamed Omar akimwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema mafanikio hayo ni kielelezo cha mageuzi chanya DIT na sekta ya elimu kwa ujumla katika kuboresha mifumo ya elimu na kuongeza ushindani kimataifa.



DIT ni miongoni mwa taasisi zinazotekeleza mradi wa kikanda wa EASTRIP, unaolenga kuimarisha elimu ya ufundi na ushirikiano na sekta ya viwanda.