Katibu Mkuu Prof Carolyne Nombo amezitaka Taasisi zinazotekeleza Mradi wa Afrika Mashariki wa Kujenga Ujuzi kwa Mlingano na Uingiliano wa kikanda (EASTRIP) kuhakikisha mradi huo wenye matokeo makubwa yenye manufaa kwa taifa unatangazwa.Ameyasema hayo katika kikao cha 11 cha Kamati Tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa EASTRIP kilichofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Jijini Dar es Salaam.Mradi wa EASTRIP wenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 172 ni wa Kikanda na unatekekezwa katika Vyuo 4 Chuo cha Usafirishaji (NIT), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Kampasi ya Dar es Salaam na Mwanza na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) .Katika Taasisi hizo kazi mbalimbali zinatekelezwa ikiweno ujenzi wa miundo mbinu, ununuzi wa Vifaa na mafunzo kwa wakufunzi ili kuwa na vituo vya umahiri katika maeneo mahsusi wanayofundisha. DIT Dar es Salaam imejikita katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Mwanza Katika Masuala ya Ngozi huku ATC ikijita katika Nishati Jadidifu na DIT usafiri anga.Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Chuo cha NIT Dkt. Prosper Mgaya ameishukuri Serikali kwa mradi huo ambapo NIT pamoja na majengo ya kituo cha umahiri na hosteli za wanafunzi wameweza kununua vifaa vya kisasa vya ufundishia masuala ya anga (mock ups).