Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Michezo na Utamaduni, Mhe. Husna Sekiboko, leo Februari 9, 2026 katika uzinduzi wa Mpango wa pamoja wa Ushirikiano kati ya Taasisi za Elimu na Viwanda unaofanyika Jijini Dar es Salaam ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mageuzi makubwa yaliyofanyika kwa muda mfupi wa kuhakikisha vijana wanapata ujuzi.



Ameeleza kuwa mageuzi haya yamekuja kushughulikia malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wadau waliokuwa wakikosoa mfumo wa elimu kwa kutoa wahitimu wasiokuwa tayari kwa soko la ajira, huku akitambua mchango wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuendeleza mchakato wa maboresho ya elimu nchini.



Amesisitiza kuwa Kamati ya Kudumu ya Bunge imejipanga kushirikiana kikamilifu na Wizara kuhakikisha Sera, Sheria na miongozo yote muhimu kwa utekelezaji wa mipango ya kuunganisha elimu na mahitaji ya viwanda inatekelezwa kwa ufanisi.