MAJUKUMU YA KITENGO ELIMU MAALUM

1 . Kusimamia utayarishaji wa Sera, Kanuni, Miongozo kuhusu mahitaji maalum ya kielimu nchini.

  1. Kusimamia kituo cha kitaifa cha huduma za kielimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum
  2. Kusimamia uandaaji mpango endelevu wa utafutaji wa rasimali kwa ajili ya kugharamia elimu kwa wenye mahitaji maalumu kuanzia ngazi ya Awali hadi Vyuo Vikuu.
  3. Kusimamia maandalizi ya miongozo kuhusu kuendeleza vipaji na vipawa vya wanafunzi kunzia Elimu ya Awali mpaka Vyuo Vikuu
  4. Kusimamia utayarishaji na uchambuaji wa data zinazohusu wanafunzi wenye mahitaji maalumu kuanzia Awali hadi Vyuo Vikuu katika mfumo wa data na sekta ya elimu na katika mtandao wazi wa Serikali na wabia na wadau mbalimbali
  5. Kusimamia uendelezaji wa mikakati ya ushrikiano baina ya Serikali/Taasisi zinazotoa huduma kwa watu wenye ulemavu na za wenye ulemavu wenyewe.

7, Kusimamia uendeshaji wa tafiti za elimu kuhusu elimu maalumu na kuzishauri wamiliki kuhusu uendeshaji bora wa taasisi husika.

  1. Kusimamia maandalizi ya viwango na mitaala inayohusu wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya elimu
  2. Kusimamia uanzishaji, uendelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi na programu kuhusu elimu maalumu.
  3. Kusimamia uandaaji na uwasilishaji taarifa za utekelezaji wa kazi kama itakavyotakiwa.

 

 KITENGO CHA ELIMU MAALUM

MGAWANYO WA MAJUKUMU YA KAZI

 

Na

Mteja

Jukumu

Huduma inayotolewa

Muda

1.

1.wanafunzi kuanzia awali hadi chuo kikuu

2. Walimu

3. Wakufunzi na

4. Wahadhiri na

 5.Watumishi wasiokuwa Walimu

6. Jamii

7. Wadau wa Elimu

8. Wazazi

Kusimamia utayarishaji wa Sera, Kanuni, Miongozo kuhusu mahitaji maalum ya kielimu nchini.

Uhamasishaji, na Uelimisha, Ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wake.

  1. Sera ya Elimu na Mafunzo yam waka 2014
  2. Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/2022-2025/2026
  3. Mwongo wa Utekelezaji wa mtaaala wa elimu ya Sekondari kwa wanafunzi viziwi kidato cha i – iv wa mwaka 2020
  4. Mwongozo rekebifu wa Utoaji Elimu kwa wanafunzi wenye Uziwikutoona 2021
  5. Mwongozo wa ubainishaji wa vipaji na vipawa vya wanafunzi wa Awali na msingi 2021
  6. Rasimu ya Mwongozo wa mwalimu na msaidizi wa mwalimu wa kufundishia darasa jumuishi 2018

 

  1. Rasimu ya Mwongozo wa usimamizi na uiendehashaji wa elimu Jumuishi Nchini 2021
  2. Rasimu ya Mwongozo wa Ziara ya Nyumbani 2021
  3. Rasimu ya mwongozo wa Shule ya Nyumbani 2021
  4. Rasimu ya Mwongozo wa mwalimu wa kufundishia wanafunzi wenye Ulemavu wa Akili hatua ya i-iii 2018
  5. Rasimu ya Mwongozo wa mwalimu wa kufundishia waanfunzi Viziwi wa darasa la i-ii 2018
  6. Rasimu ya Mwongozo wa mwalimu wa kufundishia waanfunzi wasioona wa darasa la i-ii 2018

xii. Kamusi ya Kidijiti ya  Lugha ya Alama Tanzania 2020.

xii. Rasimu ya mwongozo wa ufundishaji wa elimu jumuishi kwa walimu kazini nchini

 

 

 

 

Kusimamia kituo cha kitaifa cha huduma za kielimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum

 

  1. Ubainisjhaji na upimaji viwango vya Ulemavu kwa waanfunzi/Watoto wenye mahitaji maalum
  2. Kutoa mapendekezo ya mikondo ya kielimu stahiki kulingana na kiwango cha ulemavu. mf. Uziwi, Usonji,U/akili, Uoni U/viungo

Siku moja(1)

 

 

Kusimamia uandaaji mpango endelevu wa utafutaji wa rasimali kwa ajili ya kugharamia elimu kwa wenye mahitaji maalumu kuanzia ngazi ya Awali hadi Vyuo Vikuu.

 

 

  1. Kuwalipia Ada na fedha ya kujikimu kwa wanafunzi wenye Mahitaji Maalum
  2. Kugharamia matibabu kupitia BIMA za Afya kwa waanfunzi wenye Mahitaji Maalum
  3. Kununua na kusambaza vifaa vya kielimu na saidizi wa waanfunzi wenye Mahitaji Maalum katika ngazi zote za Elimu

Mwezi mmoja

 

 

Kusimamia uandaaji wa mwongozo wa ubainishanjia wa vipaji na vipawa vya waanafunzi

 

Kuhamasisha ushiriki wa wanafunzi wenye vipaji na vipawa wakiwemo wenye mahitaji Maalum katika mashindano ya sayansina Ubunifu.

Miezi miwili

 

 

Kusimamia utayarishaji na uchambuaji wa data zinazohusu wanafunzi wenye mahitaji maalumu kuanzia Awali hadi Vyuo Vikuu katika mfumo wa data na sekta ya elimu na katika mtandao wazi wa Serikali na wabia na wadau mbalimbali

 

kuwapatia afua stahiki kulingana na Mahitaji kama vile vifaa vya kielimu na saidizi

Mwezi mmoja (1)

 

 

Kusimamia uendelezaji wa mikakati ya ushrikiano baina ya Serikali/Taasisi zinazotoa huduma kwa watu wenye ulemavu na za wenye ulemavu wenyewe.

 

Uhamasishaji, na Uelimisha, Ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wake wa  utoaji wa huduma kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa kupitia vikao vya wadau wa Elimu Maalum na Jumuishi vya Kila mwaka wa utekelezaji wa NSIE

Siku (2)

 

 

Kusimamia uendeshaji wa tafiti za elimu kuhusu elimu maalumu na kushauri wamiliki kuhusu uendeshaji bora wa taasisi husika.

    

Kutoa ushauri wa uendeshaji bora wa taasisi husika kuhusu usimamizi na uendeshaji wa elimu maaluma na jumuishi kutokana na Tafiti zinazowasilishwa na wadau kwenye kitengo cha Elimu maalum kupitia mkutano wa mwa wa wadau

Miezi miwili (2)

 

Taasisi za serikali, dini na Binafsi na wadau mbalimbali wa Elimu

Kusimamia maandalizi ya viwango na mitaala inayohusu wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya elimu

 

    Kuwajengea Uwezo/uelewa kuhusu Elimu Jumuishi na jinsi ya kuwahudumia waanfunzi wenye Mahitaji maalum

Mwezi mmoja (1)

 

 

Kusimamia uanzishaji, uendelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi na programu kuhusu elimu maalumu.

 

Kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa miradi na programu inayohusu wanafunzi wenye Mahitaji maalum. Mf; Shule bora ESRACs (mitindo na Nkuhungu) na SWASH(Nchi nzima)

Mwaka mmoja (1)

 

 

Kusimamia uandaaji na uwasilishaji taarifa za utekelezaji wa kazi kama itakavyotakiwa.

 

Kutatua changamoto za waanfunzi wenye mahitaji maalumu kuazia ngazi ya Awali hadi Vyuo Vikuu zilizojitokeza kulinga na na taarifa husika mf. Upungufu ewa vifaa vya kielimu na saidizi pamojka na miundombinu. 

Siku 2