Katika kuunga mkono juhudi za Serikali, zinazotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na wadau katika kuimarisha Elimu Amali, Mbunge wa Moshi Mjini, Mhe. Ibrahim Shayo, ameahidi kufadhili masomo ya vijana 10 kila mwaka katika Chuo cha VETA Moshi.



Mhe. Shayo ametoa ahadi hiyo Januari 07, 2026 mkoani Kilimanjaro baada ya kujionea mafanikio ya chuo hicho katika kutoa elimu ya vitendo inayowawezesha vijana kupata ajira ndani na nje ya nchi.



Ameeleza kuwa hatua hiyo ni fursa kwa vijana wa Moshi Mjini kujijengea ujuzi, kuboresha maisha yao na kuchangia maendeleo ya taifa