Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Dtk. Richard Masika ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Taasisi hiyo Mradi wa TELM II ambao umelenga kuanzisha Kituo cha Ujasiriamali, Ubunifu na Uhawilishaji wa Teknolojia.



Dkt. Masika ametoa shukrani hizo Disemba 5, 2025 jijini Dar es Salaam akizungumza katika Mahafali ya 19 ya Taasisi hiyo duru ya kwanza, amesema katika mwaka wa fedha 2025/26, Serikali imetenga zaidi ya Sh. Bilioni mbili kwa ajili ya ukarabati wa jengo la Kituo hicho.



Kumbuka Mradi huo wa miaka miaka mitano (2025/2030) unatekelezwa kwa bajeti ya Euro milioni 19.79 (sawa na Sh. Bilioni 54). Fedha hizo ni mkopo nafuu kutoka Serikali ya Italia kwa Serikali ya Tanzania kupitia makubaliano rasmi.



Taasisi zingine zinazonufaika na Mradi wa TELMS II, ni Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST).

Maeneo mengine, Mradi huo unalenga kuimarisha maendeleo ya nishati endelevu pamoja na suala la uhifadhi mazingira.