Naibu Karibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi Septemba 19, 2025 amekagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)
Kampasi ya Mizengo Pinda Katavi.



Mradi huo unatekelezwa chini ya Mradi wa Elimi ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) Kwa gharama ya Sh. bilioni 17.4



Kutokana na uwekezaji huo mkubwa unaofanywa na Serikali Prof. Mushi ameuagiza uongozi wa Chuo hicho kuandaa programs za kuvutia na zenye tija kwa jamii ya Mkoa wa huo, mikoa jirani na Taifa kwa ujumla.



Aidha, amewataka wasimamizi wa mradi kutekeleza haraka maagizo aliyoyatoa kuboresha mapungufu machache yaliyobainika ili thamani ya fedha iliyowekezwa iweze kupatikana na kuwanufaisha watanzania.



Naye, Rasi wa Ndaki hiyo Prof. Anna Sikila ameishukuru Serikali kwa kutekeleza Mradi huo utakaonufaisha Wanafunzi wapatao 2,000 na kwamba uongozi huo utatekeleza maagizo yote kukamilisha Mradi kwa mafanikio.



Mhandisi Mshauri Elia Mwamlima, amesema Mradi huo unahusisha majengo ya taaluma ikiwa na maktaba za TEHAMA, maabara na kumbi za mihadhara pamoja na hosteli.