Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema kumudu lugha na kuimarisha ujuzi wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kutawawezesha wanafunzi kuelewa vyema kila wanachofundishwa na hivyo kufanikisha malengo ya elimu.



Akizungumza Januari 29, 2026, Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa watoto wa elimu ya awali na wanafunzi wa Darasa la kwanza na la pili.



Chalamila ameeleza kuwa mpango unaozinduliwa utakuwa chachu ya mafanikio makubwa katika elimu na umahiri wanafunzi katika mafunzo kadri wanavyoendelea