
Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi,amezitaka Taasisi za elimu ya juu nchini kuimarisha tafiti na ubora wa elimu kwa kushirikisha Sekta binafsi,hasa katika Sayansi na Teknolojia, ili kuongeza ubunifu na kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji.

Mhe. Nchimbi ametoa maagizo hayo Februari 9, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa pamoja wa Ushirikiano kati ya Taasisi za Elimu na Viwanda ili kuhakikisha vijana wanaohitimu wanakuwa na ujzi unaohitajika katika soko la ajira.

Pia amewataka waajiri na Viwanda kushiriki kikamilifu katika mapitio ya mitaala, kutoa nafasi za mafunzo kwa vitendo, uanagenzi na mafunzo kazini.

"Wataalamu kutoka viwandani mnapaswa kushiriki moja kwa moja katika ufundishaji na tathmini ya wanafunzi ili kuhakikisha ujuzi unaopatikana unalingana na mahitaji ya soko.

Mhe. Nchimbi pia amezitaka Taasisi za elimu na Sekta binafsi kuzingatia kasi ya uuaji wa maendeleo sayansi na teknolojia duniani kwa kubaini ujuzi muhimu unaohitajika sasa na baadaye na kutaka Mpango huu utekelezwe kivitendo na kuleta matokeo yanayopimika katika ubora wa mafunzo, ajira za vijana, ubunifu na ukuaji wa uchumi wa taifa.


