
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, ameongoza majadiliano kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Balozi wa Falme za Kiarabu (UAE) nchini, Mhe. Khalifa Abdulrahman Almarzouqi, kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kielimu kati ya nchi hizo mbili.

Majadiliano hayo yamefanyika Januari 9, 2026 jijini Dar es Salaam, yamelenga kuongeza fursa za ufadhili wa masomo katika fani za Sayansi ya Data, Akili Unde na Sayansi Shirikishi na kuendeleza miundombinu ya elimu, tafiti za kisayansi, ubunifu na matumizi ya teknolojia. Pande zote zimeeleza dhamira ya kuendeleza ushirikiano wa kimkakati utakaokuza rasilimali watu yenye maarifa na ujuzi.

Kikao hicho pia, kimehudhuriwa na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na baadhi ya Wakuu wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati nchini.


