Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Hussein Mohamed Omar amefunga Kikao cha Pamoja kati ya Serikali na Benki ya Dunia (Joint Mission Meeting) kuhusu utekelezaji wa Miradi ya Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) na Mpango wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST).



Kikao hicho cha Siku tatu kilianza Oktoba 15 hadi 17, 2025 kimejadili mafanikio katika utekelezaji wa Miradi hiyo miwili, changamoto na mikakati katika kushughulikia baadhi ya changamoto zilizojitokeza ili kukamilisha miradi hiyo kwa ufani na wakati.



Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Ndg. Atupele Mwambene