Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda aungana na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar kuaga mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi, ambaye alifariki Dunia Februari 29, 2024 katika Hospital ya Mzena jijini Dar es Salaam.