1.0 Utangulizi
Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi na Ugavi kina jukumu la kusimamia ununuzi wa vifaa, na huduma kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi Sura 410 na Kanuni zake (G.N Na.518) za mwaka 2024. Kitengo pia kina jukumu la kusimamia na kuratibu ununuzi wa vifaa na huduma kwa kutumia fedha za matumizi ya kawaida pamoja miradi inayofadhiliwa na wadau wa maendeleo kama (ESPJ, SEQUIP, TESP, GPE-TSP, BOOST, SWASH, EP4R, HEET, EASTRIP, THELMS, EPIPT na UTC).
2.0 Majukumu
Katika kutekeleza majukumu yake kitengo kinafanya kazi zifuatazo:-
- Kumshauri Afisa Masuuli kwenye masuala yanayohusu Ununuzi na Ugavi;
- Kushauri Menejimenti kwenye masuala yanayohusu Ununuzi na Ugavi;
- Kusimamia ununuzi wa bidhaa na huduma mbalimbali;
- Kuratibu Vikao vya Bodi ya Zabuni ya WyEST;
- Kutekeleza maamuzi ya Bodi ya Zabuni ya WyEST;
- Kutayarisha Mpango wa Ununuzi wa Mwaka wa shughuli za WyEST pamoja na za miradi ya maendeleo;
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya Wizara;
- Kuandaa nyaraka za zabuni;
- Kuandaa matangazo ya zabuni na kutangaza zabuni mbalimbali kwenye mfumo wa NeST;
- Kuandaa nyaraka za mikataba ya ununuzi;
- Kutunza kumbukumbu zote za michakato ya ununuzi;
- Kuandaa taarifa za ununuzi za kila mwezi na taarifa za utekelezaji wa Mpango wa Ununuzi kila robo mwaka;
- Kuhifadhi orodha au rejista ya mikataba yote iliyosainiwa;
- Utunzaji wa vifaa na kuratibu ufutaji wa vifaa chakavu (disposal of public assets) pamoja na kuhuisha Daftari la Mali (Assets Register) kwa kutumia mfumo wa GAMIS;
- Kufanya uhakiki na kuhesabu ya mali za kudumu za Wizara kwa kila mwaka; na
- Kusimamia na kuhakikisha ubora unapatikana katika bidhaa, huduma na kazi za ujenzi.





