Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) amewasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 leo Mei 07, 2026 wakati wa Kikao cha 24 cha Mkutano wa 3 wa Bunge la 13 jijini Dodoma.



Aidha, Mhe. Asha Feruzi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, amewasilisha taarifa ya Kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato ja Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.