Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga amewataka wahandisi wanaosimamia ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Mwanga kuongeza idadi ya mafundi ili kuharakisha ujenzi wa VETA hiyo ya Wilaya na kuongeza kuwa uwepo wa nguvu kazi ya kutosha kutafanikisha ujenzi kukamilika kulingana na ratiba.

Ametoa agizo hilo Novemba 16, 2023 wilayani Mwanga, Mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya ukaguzi na ufuatiliaji wa hatua za ujenzi wa Chuo hicho.Aidha Mhe. Kipanga ameagiza kufanyika tathmini na maamuzi ya haraka juu ya kudhibiti mkondo wa maji unaopita katika eneo hilo la ujenzi na kupatiwa uvumbuzi wa haraka ukizingatia kipindi hiki ni cha mvua kubwa.Pia awataka mafundi kuwa na ufanisi kwenye kufuata vipimo halisi vya kwenye michoro na kuzingatia mazingira.