1. 1.   UTANGULIZI

Ofisi ya Kamishna wa Elimu ina jukumu kubwa katika kuboresha Mfumo wa Elimu nchini ambayo hutegemewa kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Ofisi hii hutekeleza majukumu yake kwa kuhakikisha kuwa Elimu inayotolewa inakidhi viwango vya Kimataifa yenye kuwajengea wanafunzi maarifa, ujuzi na maadili yanayohitajika katika karne ya 21. 

  1. 2.   MUUNDO WA OFISI YA KAMISHNA WA ELIMU

Ofisi hii ina jumla ya Wakurugenzi wawili (2) ambao ni Mkurugenzi Elimumsingi (DBE) na Elimu Maalum (DSNE) pamoja na Wakurugenzi Wasaidizi watatu (03) ambao ni Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Ualimu (ADTT), Uendelezaji wa Sera ya Elimumsingi (ADPD) na Ithibati ya Shule (ADSA). Kamisheni ya Elimu inaundwa na Idara/sehemu na Vitengo mbalimbali vinavyosimamiwa na Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi kama ifuatavyo:

  1. i.   Idara ya Elimu Msingi;
  2. ii.  Sehemu ya Elimu ya Ualimu;
  3. iii. Kitengo cha Elimu Maalum;
  4. iv. Sehemu ya Uendelezaji wa Sera ya ElimuMsingi; 
    1. a. Elimu ya Awali
    2. b. Elimu ya Msingi 
    3. c. Elimu ya Sekondari 
    4. d. Masuala Mtambuka
    5. e. Elimu ya watu wazima; na 
  5. v.  Sehemu ya Ithibati ya Shule.

3.   MAJUKUMU YANAYOTEKELEZWA NA OFISI YA KAMISHNA WA ELIMU

Ofisi ya Kamishna wa Elimu inayo majukumu mbalimbali yanayotekelezwa kulingana na Sheria ya Elimu Sura 353 kama ifuatavyo: -

  1. 1.  Kutunga na kufanya mapitio ya Sera, Nyaraka pamoja na Miongozo mbalimbali inayohusu Elimumsingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu;
  2. 2.  Kusimamia uendelezaji wa mikakati ya ushrikiano baina ya Serikali/Taasisi zinazotoa huduma kwa watu wenye ulemavu na za wenye ulemavu wenyewe.
  3. 3.  Kuandaa, kutoa ithibati na kufanya mapitio ya mitaala, mihtasari, vitabu na vifaa mbalimbali vya elimu kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania;
  4. 4.  Kusimamia uandaaji na uendeshaji wa mitihani ya upimaji ya Kitaifa hapa nchini kupitia Baraza la Mitihani Tanzania;
  5. 5.  Kusimamia utoaji na uendeshaji wa mafunzo ya awali kwa walimu tarajali na mafunzo kazini kwa walimu na wakufunzi;
  6. 6.  Kusajili Vyuo vya Ualimu na Shule za Serikali na Zisizo za Serikali;
  7. 7.  Kuendeleza Elimumsingi kwa kutoa Ithibati ya Mafunzo ya Ualimu na Maendeleo ya kitaalamu ya Walimu;
  8. 8.  Kuweka Viwango vya Taaluma ya Ualimu;
  9. 9.  Kusimamia utoaji wa Huduma za Maktaba nchini kwa kushirikiana na Bodi ya Huduma za Maktaba (BOHUMATA); na
  10. 10 Kusimamia utoaji wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW).

ORODHA YA SHULE ZINAZOTOA ELIMU YA AMALI-2025

MPANGO MKAKATI WA KISAYANSI WA KUJENGA UMAHIRI WA KUSOMA, KUANDIKA NA KUHESABU (KKK) KWA WATOTO WA ELIMU YA AWALI NA WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA NA LA PILI

WARAKA WA ELIMU NA. 4 WA MWAKA 2022 KUHUSU UIMARISHAJI WA MAZINGIRA YA SHULE KUWA SALAMA NA WEZESHI KATIKA UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI

WARAKA WA ELIMU NA. 02 WA MWAKA 2023 KUHUSU UTOAJI WA HUDUMA YA KULAZA WANAFUNZI BWENI KWA NGAZI ZA ELIMU YA AWALI NA SHULE ZA MSINGI

WARAKA WA ELIMU NA. 03 WA MWAKA 2025 KUHUSU MFUMO WA KITAIFA WA KUWEZESHA SHULE KUWA JUMUISHI ZAIDI

WARAKA WA ELIMU NA. 24 WA MWAKA 2002 KUHUSU ADHABU YA VIBOKO

WARAKA WA ELIMU NA 05 WA MWAKA 2025 KUHUSU KALENDA YA MIHULA YA MASOMO KWA SHULE ZA AWALI, MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2026