Serikali imesema kuwa ipo tayari kushirikiana na Taasisi yeyote katika kuhakikisha vijana na wanataaluma wanapata fursa za kusoma nje ya nchi.

Haya yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga Januari 28, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa elimu na mabalozi wa nchi mbalimbali wa kujadili fursa za ufadhili wa masomo katika nchi zao.



Mhe. Kipanga amesema kuwa Tanzania siyo kisiwa, hivyo kuna wajibu wa kuhakikisha kuna mwingiliano wa kielimu kati ya Tanzania na nchi nyingine duniani kwa kutafuta ufadhili wa vijana kwenda kupata ujuzi na umahiri na kuruhusu watu wa nchi nyingine kuja nchini kwa ajili ya kupata elimu.



"Mkutano huu umetukutanisha wadau wa elimu kuhakikisha tunatafuta fursa za ufadhili kwa vijana na wanataaluma kwa ajili ya kwenda kuongeza ujuzi katika mbalimbali Duniani" amesisitiza Mhe. Kipanga

Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa vijana hao watakapokwenda masomoni na kurudi nchini watalisaidia taifa kupitia ujuzi na umahiri walioupata katika maeneo ya kipaumbele kama vile Kilimo, Umeme, Maji na maeneo mengine.

Mkurugenzi wa Bright Famius Company LTD, Robert Matoke amesema taasisi yake imeandaa mkutano huo ili kuwawezesha vijana wa kitanzania kupata taarifa za fursa mbalimbali za masomo zinazotolewa na balozi zilizopo nchini kwani mara nyingi vijana wamekuwa hawapati taarifa juu ya uwepo wa fursa hizo



Ameongeza kuwa katika mkutano huo Balozi za Marekani, Uingetezaa, ufatansa na Indonesia wamepata nafasi ya kuelezea fursa za ufadhili ambazo zinaweza kuombwa na vijana wa Tanzania

Naye Koingozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo akikuu cha Dar es Salaam Ally Ahmad amesema Serikali ya Wanafunzi DARUSO itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kupata fursa zaidi za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wanaotaka kujiendeleza zaidi mara wanapomaliza shahada zao za kwanza.