
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, leo Oktoba 14, 2025, ameungana na Watanzania katika Maadhimisho ya Uzimaji wa Mwenge wa Uhuru yaliyofanyika mkoani Mbeya.

Tukio hilo ni ishara ya kuhitimisha mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu, ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo imezinduliwa na kukaguliwa katika mikoa mbalimbali nchini.


