Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, leo Septemba 24, 2025, amefanya ukaguzi wa awali wa Maonesho ya wadau mbalimbali yanayofanyika katika Mkutano wa Kimataifa wa Kujadili Ubora wa Elimu.



Mkutano huo wa siku tatu, umeandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), na umewakutanisha washiriki kutoka sekta za umma, binafsi, na mashirika ya kimataifa ili kuchochea majadiliano ya kitaalamu kuhusu upatikanaji wa rasilimali za ndani, Kwa ajili ya Elimu Bora, jumuishi na Endelevu barani Afrika



Mkutano huo, unatarajiwa kufunguliwa rasmi na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko.