PWANI

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga amewahimiza wasimamizi wa mradi wa Ujenzi wa VETA ya Wilaya ya Kibiti na Mkuranga kukamilisha hatua kwa Hatua na kufuata Kanuni za Ujenzi wa Miradi Hiyo kwa wakati na kuwataka kufanya marekebisho katika maeneo yenye Changamoto zilizobainika.

Mhe. Kipanga ametoa rai hiyo March 26, 2024, akiwa katika ziara ya Kukagua na kufanya tathmini ya ujenzi wa VETA hizo ikiwa ni miongoni Mwa VETA 63 zinazojengwa na Serikali nchini.



Katika hatua nyengine MHE QS KIPANGA amefurahishwa na kuwapo kwa Mhandisi, mshauri uelekezi na Afisa Manunuzi wa Halmashauri zilizo na Miradi ya VETA kuwepo eneo la ujenzi wakati wote ili kuhakikisha mafundi wanajenga kwa ufanisi na kufuata taratibu zote za ujenzi.

*"Nimefurahishwa na uwepo wa mafisa Hawa wasaidi kutoka Halmashauri za Kibiti na Mkuranga, Wilaya zote zenye miradi ya VETA watalamu hao wawepo Eneo la mradi kwa ajili ya kutoa Msaada kwa mafundi na Wataalamu Wengine wa DIT,MUST nk*" alisisitiza MHE QS KIPANGA



Aidha Amefurahishwa na umakini kwa mafundi wanaojenga karakana na madarasa ya VYUO hivyo kufuata maelekezo yote wanayopewa na wahandisi sambamba na vipimo na michoro iliyopo kwenye ramani za ujenzi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Kibiti Ndg DENISI KITALI ameishukuru Serikali kwa kutenga fedha za Ujenzi wa chuo Cha VETA Kibiti kata ya Bungu Kijiji Cha Nyambili na kumshukuru Naibu Waziri huyo kwa kufanya ukaguzi, tathmini na kushauri,



*"Binafsi Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Kibiti Pamoja wananchi tunamshukuru MHE DKT SAMIA SULUHU HASSAN Kwa kutupatia miradi ya Maendeleo mingi Hapa Kibiti pamoja nawe pia kwa Kufanya Ukaguzi wa Hali ya juu kwa kweli tumepata somo kubwa kwako*" alifafanua Ndg DENISI KITALI.