Serikali ya Uingereza itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha sekta vya elimu nchini.



Hayo yameelezwa na Waziri wa Maendeleo na Afrika wa Uingereza Mhe Andrew Mitchell alipokutana na kufanya Mazungumzo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda April 5, jijini Dodoma.



Katika kikao hicho ambacho pia kilimhusisha Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, wamejadiliana juu ya afua mbalimbali ambazo zinajenga ustawi wa watanzania katika elimu na afya



Katika mazungumzo hayo waziri Mkenda ameeleza umuhimu wa kushirikiana katika kutekeleza Sera na Mitaala mipya akisisitiza juu ya mafunzo ya amali na kuhakikisha watoto wote wa kitanzania wanapata elimu bora katika mazingira bora.



Waziri Mitchell amepongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua za mageuzi katika elimu akieleza kuwa mafunzo ya amali yanakwenda kuwa chachu ya kujenga vijana wenye ujuzi na hivyo kuongeza nguvu kazi katika sekta mbalimbali, uzalishaji na hivyo kukuza uchumi.