
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, leo Septemba 22, 2025 amefanya ziara katika Kituo cha Umahiri cha Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu kilichopo Mloganzila, kinachomilikiwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Katika ziara hiyo, Prof. Nombo amejionea vifaa vya kisasa vinavyotumika katika ufundishaji na ujifunzaji kwa lengo la kuboresha ujuzi wa wataalamu wa afya nchini, ambapo amesisitiza umuhimu wa kuvilinda na kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kudumu kwa muda mrefu na kuendelea kutoa huduma bora bila kupoteza ubora wake.
“Vifaa hivi ni rasilimali muhimu kwa maendeleo ya sekta ya afya. Ni wajibu wa MUHAS kuhakikisha vinatunzwa kwa uangalifu ili viendelee kutoa mchango mkubwa katika mafunzo ya wataalamu wetu,” alisema Prof. Nombo.
Kituo hicho cha umahiri ni miongoni mwa jitihada za serikali na wadau wa maendeleo katika kuboresha elimu ya afya na kuongeza ufanisi wa huduma za matibabu kwa wananchi