Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Februari 20, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na washiriki wa Kongamano la Kwanza la Kimataifa Kuhusu Dhima ya Lugha za Asili katika Kujenga Tamaduni - Mtambuka, Diplomasia ya Kiisimu ya Kiuchumi.



Prof. Mkenda ameongeza kuwa kwa sasa Serikali imeanzisha Tuzo ya Uandishi Bunifu zinazojulikana kama Tuzo za Mwalimu Julius Nyerere zinazotolewa katika maeneo ya Hadithi fupi, tamthilia na hadidhi za watoto ambazo zimeanza mwaka 2023.



Ameongeza kuwa hata katika mabadiliko ta Mitaala kumeongezwa lugha nyingi zaidi zinazofundishwa kwa hiari zikiwemo Kiarabu, Kifaransa na Kichina ambapo Mwanafunzi wa Elimu ya Msingi anaweza kuchagua kuzisoma na kuwa selikali itaendelea kutafakari zaidi ili kuongeza lugha nyingine na kuhakikidha lugha zinachangia katika Diplomasia ya kiisimu kiuchumi.