Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Februari 9, 2026, jijini Dar es Salaam amezindua Mpango wa Ushirikiano kati ya Taasisi za elimu na Viwanda unaolenga kulinganisha mafunzo na mahitaji halisi ya soko la ajira.



Mhe Nchimbi amesema Mpango huu ni utekelezaji wa ahadi ya Serikali kuhakikisha elimu inayotolewa inakidhi mahitaji ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, sambamba na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020–2025.