Taasisi ya Sayansi ya Bahari (IMS) ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam iliyopo Buyu Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,
Naibu katibu Mkuu Sayansi na Teknolojia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi amekutana na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar Ndugu Khamis Abdullah Said na kujadiliana kuhusu kuimarisha utoaji Elimu ya Juu kwa kuzingatia mabadiliko ya kisera na uchangamano wa kikanda.



Mazungumzo yamefanyika Septemba 26, 2025 Zanzibar katika Ofisi za Wizara ya Elimu navMafunzo ya Amali.



Viongozi hao wamekubaliana juu ya umuhimu wa kuwa na mifumo madhubuti ya kuratibu elimu ya juu ili kuandaa rasilimali watu wenye ujuzi, maarifa na uwezo wa kukabiliana na mahitaji ya soko la ajira la sasa na baadae kitaifa na kimataifa.