
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima kutoka Chuo Kikuu cha Jimbo la Nasarawa, Keffi nchini Nigeria kwa njia ya mtandao, tarehe 11 Aprili, 2026 Ikulu, Dodoma.

Mhe. Rais ametunukiwa Shahada hiyo ya Uzamivu ya Heshima kwa kutambua mchango wake kama Kinara wa Nishati Safi ya Kupikia, Afya ya Mama na Mtoto, Taswira nzuri katika masuala ya Uongozi kwa Wanawake Afrika na Kusimamia Masuala ya Biashara hususani kwa Vijana Afrika.

Katika hafla hiyo Viongozi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia wameshiriki wakiongozwa na Waziri Prof. Adolf Mkenda.

Kwa niaba ya Uongozi na watumishi wa Wizara tunampongeza Rais wetu kwa kutunukiwa Shahada hiyo ya heshima.


