
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, Prof. Penina Mlama, amesema kuwa majaji wamekamilisha kazi ya kusoma miswada 260 na tayari orodha teule imepatikana, ikihusisha washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania pamoja na washiriki wapya kutoka nje ya nchi.

Akizungumza na vyombo vya habari Aprili 8, 2026 jijini Dodoma, Prof. Mlama amesisitiza kuwa mwitikio wa mwaka huu umekuwa mkubwa na ni ishara ya hamasa ya waandishi kushiriki katika kukuza fasihi na uandishi bunifu.

Ameongeza kuwa Washindi wa kila nyanja watatangazwa rasmi Aprili 13, 2026 na kuzawadiwa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu na vyeti
Amesema kuwa mshindi wa kwanza, muswada wake utachapishwa na Serikali itanunua nakala kwa ajili ya shule na maktaba za taifa ili kuendeleza fasihi na kuhamasisha uandishi bunifu nchini.


