Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo wameendelea na mafunzo maalum yanayofanyika katika Ofisi ya Bunge jijini Dodoma, yakilenga kuwaongezea uelewa kuhusu masuala muhimu ya sekta ya elimu nchini.



Tarehe 11 Februari 2026, wajumbe hao wamekutana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kupatiwa maelezo kuhusu usimamizi na uendeshaji wa Vyuo vya kati na vyuo vikuu nchini pamoja na Mamlaka ya Elimu Tanzania.



Mafunzo hayo yamelenga kuimarisha ufanisi wa uendeshaji wa taasisi hizo, kuboresha ubora wa elimu inayotolewa pamoja na kuongeza uwajibikaji katika elimu ya juu.



Mawasilisho yametolewa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) pamoja na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)