Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, amehimiza wasichana kupenda masomo ya sayansi na kushiriki kikamilifu katika taaluma hizo kutokana na manufaa yake kwa maisha yao na maendeleo ya taifa.



Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi yaliyofanyika jijini Dodoma Februari 11, 2026, Mhe. Mahundi amesema sayansi inawawezesha wanawake na wasichana kujenga uwezo wa kiuchumi na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.



Mhe. Mahundi amebainisha kuwa, Serikali inaendelea kutekeleza mikakati ya kuondoa vikwazo vinavyowazuia wanawake na wasichana kushiriki katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi ili kuleta usawa wa kijinsia