
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Emmanuel Nchimbi amewahakikishia watanzania kuwa Serikali itaendelea kusimamia sekta ya elimu na kuhakikisha elimu inayotolewa inaendelea kuwa bora.

Akizungumza leo Februari 05, 2026 mara baada ya kufanya ziara katika Chuo cha VETA Chemba , Dodoma Mhe. Dkt. Nchimbi amesema kuwa amefurahishwa sana kuona mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji yalivyoboreshwa na kwamba hii inafanya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kuwa na tija zaidi na yenye mafanikio kwa watanzania.

“Nimefurahishwa kwa dhati na utekelezaji huu wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi na maelekezo ya Rais wetu kuhusu kuboresha elimu nchini, majengo ya Chuo hiki ni mazuri na vifaa vya kisasa. Katika karakana mbili nilizotembelea vijana wale wameonesha ujuzi na umahiri walio nao katika kutumia vifaa vile ya kujifunzia.”amesema Dkt. Nchimbi.

