
Utekelezaji wa Sera ya elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 na Ilani ya Chama cha Mapinduzi unachangia kwa kiasi kikubwa katika kuwezesha Tanzania kupata rasilimali watu mahiri, bunifu na wenye stadi zinazohitajika.

Hayo yamesemwa Februari 5, 2026 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Wanu Hafidh Ameir wakati wa ziara ya Makamu wa Rais katika Chuo cha VETA Chemba jijini Dodoma.

Amesema nia ya Serikali ni kuona vijana wanapata ujuzi kulingana na mazingira ya nchi na soko la ajira akiitaja Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi ( VETA) kama Taasisi mojawapo iliyojikita katika kutoa elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Ili kuhakikisha azma ya kupata vijana wenye ujuzi inafikiwa


