
Washirika wa Maendeleo katika Elimu (Development Partners) wamekutana na Uongozi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknojia na Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI jijini Dar Es Salaam kujadili mfumo wa ufadhili wa elimu unaozingatia matokeo (Result Based Financing for Education ( EP4R).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, ameongoza ujumbe wa Wizara walioshiriki kikao hicho kilichofanyika tarehe 2 Februari 2026.

Washiriki katika kikao hicho pamoja walijadili umuhimu wa kuratibu kwa pamoja uwekezaji katika sekta ya elimu kwa kuzingatia vipaumbele na matokeo lengwa kitaifa.


