Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, tarehe 28 Januari 2026 kupitia Televisheni ya Taifa (TBC1), wamewaalika Watanzania kushiriki katika uzinduzi wa Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kwa watoto wa Elimu ya Awali na wanafunzi wa Darasa la Kwanza na la Pili.