
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ameeleza kuwa Wizara na Taasisi zilizo chini yake zimekutana jijini Dodoma Januari 20, 2026 kuangalia utekelezaji wa Malengo 2025/26 na kuweka mikakati ya pamoja ya kuwezesha ufikiaji malengo ya Dira 2050 katika sekta za Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Ameeleza kuwa moja ya mikakati itakayojadiliwa ni kuhusu utekelezaji wa elimu ya lazima ya miaka kumi na uimarishaji mafunzo ya amali katika ngazi ya sekondari, kuimarisha fursa za mafunzo ngazi ya elimu ya juu na ufadhili.

Ameongeza pia kikao hicho cha kimkakati kitajadili pia programu zingine za elimu zenye lengo la kuimarisha Sekta.


