
Walimu wa Mkoa wa Geita wametoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuthamini kada hiyo na kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta ya elimu.
Akizungumza Oktoba 03, 2025 katika Maadhimisho ya Siku ya Walimu kwa Wilaya ya Bukombe Katibu Mkuu Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Geita Pauline Ntinda amesema kuwa jitihada hizo zimeongeza morali ya kazi, kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, na kuimarisha usimamizi wa elimu katika mkoa huo.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2021-25, Mkoa huo umepokea takriban Sh. Bilioni 20 kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya shule, ikijumuisha madarasa 134, nyumba za walimu 103, matundu ya vyoo 332, maabara na maktaba. Shule tatu mpya za sekondari zimejengwa, na vifaa vya TEHAMA kama projekta, kompyuta pakato, smartboards na mashine za kudurufu vimesambazwa kwa shule za sekondari.
Ameongeza kuwa Serikali imetoa kibali cha upandishaji madaraja kwa walimu 823 na kubadilisha miundo ya utumishi kwa walimu 737 ndani ya mwaka wa fedha 2024/2025. Walimu wa kujitolea 604 wanaolipwa kupitia mradi wa GPE-TSP wamepangwa katika shule za pembezoni, sambamba na ujenzi wa nyumba za walimu. Ajira mpya zimeendelea kutolewa kila mwaka, ambapo walimu 607 waliagizwa mkoani Geita mwaka 2023/2024, na walimu 770 wamepangwa kwa mwaka wa fedha 2024