Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI leo Septemba 26, 2025 wamefanya kikao kazi jijini Dodoma kwa ajili ya kupokea na kujadili utekelezaji wa Mradi wa Secondary Education Quality Improvement Program (SEQUIP).



Katika kikao hicho, pande zote mbili zilikubaliana kuendeleza ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa ufanisi na kuleta matokeo chanya katika sekta ya elimu nchini.



Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Elimu kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Emmanuel Shindika, pamoja na maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Elimu, taasisi zilizo chini ya wizara hiyo na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).