
Tanzania imekuwa Mwenyeji wa Mkutano wa 20 wa Kisekta wa Mawaziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Utamaduni na Michezo ambao umefanyika Jijini Dar es Salaam Septemba 23, 2025
Mkutano huo ambao Mwenyekiti wake ni Waziri wa Elimu kutoka Kenya umehudhuriwa na wajumbe kutoka nchi wanachama ambapo ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Aftika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amemwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda katika Mkutano huu ambao unajadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta za Elimu, Sayansi, Teknolojia, Utamaduni na Michezo