
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi Septemba 18, 2025 amekagua maandalizi ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kisomo Kimataifa na Juma la Elimu ya Watu Wazima yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kashaulili Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.
Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.